Soma hapa jinsi ya kuwa na nguvu za kiume za kutosha pasipo hata kutumia DAWA

Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume haraka Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana. Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili. Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’ . Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha. Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku. Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume haraka 1. Ndizi Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa. Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi ( libido). 2. Tikiti maji Matikiti maji ni tunda muhimu sanna kwa kulinda ndoa inatakiwa walau kwa siku upate vipande viwili au vitatu na sasa yapo kwa wingi ushindwe wewe na ni muhimu ukala na mbegu zake. Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B6,C. Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi. Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu . Faida nyingine 12 za tikiti maji kiafya ukiacha hii ya nguvu za kiume • Asilimia 92 yake ni maji • Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho • Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili, • Huponya majeraha, • Hukinga uharibifu wa seli • Huboresha afya ya meno na fizi • Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema • Hubadilisha protin kuwa nishati • Chanzo cha madini ya potasiamu • Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la damu • Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini • Huondoa sumu mwilini Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya mara hivi mara kwa mara. 3. Unga wa Mbegu za maboga Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado. Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume. Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukimwaga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo. Soma pia hii > Magonjwa hatari 10 yanayotibika kwa kutumia mbegu za maboga 4. Kitunguu swaumu Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi. Sifa kuu za kitunguu saumu zinazokifanya kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kuwa na viasili kadhaa ambavyo vina uwezo tofauti tofauti. Baadhi ya viasili hivi husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu ( vasodilation kwa lugha ya kiingereza) kwa kubadilisha polysulphides zilizo ndani yake kuwa hydrogen sulphides kwenye seli nyekundu za damu. Pia, kitunguu saumu husaidia kuthibiti kiwango cha kemikali iitwayo homocystine mwilini na hivyo kupunguza madhara ya kisukari. Kitunguu saumu kina allicin , kiambato ambacho husaidia mwili kuwa na mzinguko mzuri wa damu hadi kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na damu ya kutosha katika uume husababisha hiki kiungo kusimama na hivyo kustaimili tendo la ndoa kwa muda mrefu. Namna ya kutumia kitunguu swaumu: 1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja 2. Kigawanyishe katika punje punje 3. Chukua punje 6 4. Menya punje moja baada ya nyingine 5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10 6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi. Fanya hivi kila baada ya siku 1 unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4. Unaweza pia kuendelea kukitumia hata kama unmepona tatizo lako. Ukiona kichwa kizito au kinauma pumzika kutumia kitunguu swaumu kwa siku 3 hivi kisha endelea tena, mhimu usitumie kila siku bali ni kila baada ya siku 1. Soma pia hii > Jitibu magongwa 30 kwa kutumia kitunguu swaumu 5. Siagi ya Karanga Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi. Siagi ya karanga ina kiasi kingi cha mafuta masafi yasiyoweza kusababisha kolesto/lehemu mwilini (unsaturated fats) na kiasi kingi cha protini, vitu hivi viwili vinafanya kazi ya kuongeza nguvu mwilini. Siagi ya karanga ina kalori nyingi zitakazokuwezesha ubaki ni mwenye nguvu kutwa nzima. Kwakuwa ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, shaba, magnesium, na potasiamu, siagi ya karanga ni nzuri sana katika kuuweka katika usawa mzuri mzunguko wa damu mwilini. Kadharika kiasi kingi cha protini kilichomo kwenye siagi ya karanga kinasadikika kuwa na uwezo wa kuongeza nguvu au uwezo wa mwili na kutengeneza mishipa mingi na imara zaidi. Kaanga kidogo karanga bila kuziunguza na usizitie chumvi, kisha zimenye au ondoa maganda yake. Saga kwenye blenda huku ukiongeza kidogo kidogo mafuta yoyote ya mboga mboga kama ya alizeti au mafuta ya karanga, ongeza sukari au asali kidogo na chumvi kidogo. Mimi napenda zaidi kuitumia kwenye mkate lakini pia unaweza kuongeza siagi ya karanga kwenye karibu kila mboga ya majani, samaki na kadharika. Ukiacha radha yake nzuri na tamu, siagi ya karanga ni chakula chenye afya na nguvu nyingi na isiyo na takataka zozote zisizohitajika na mwili. Soma na hii > faida 12 za siagi ya Karanga kiafya 6. Parachichi Chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongezamajimaji yenye utelezisehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana. Hili ni tunda ambalo watafiti wamebaini kwamba lina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume. Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E. Vitamini E husaidia katika uzalishaji wa homoni zinazosaidia kuongeza nguvu za kiume. Kulingana na watafiti tofauti, watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali haswa wakati wa kufanya mapenzi. Pia, faida za tunda hili haziengemei upande wa wanaume pekee. Katika upande wa wanawake, tunda hili husaidia kuongeza majimaji yaliyo na utelezi katika sehemu za siri za mwanamke ili kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa tendo la ndoa. 7. Pilipili Pia pilipili unaweza changanya kwenye chakula au ukala hivyo hivyo kwani zinasaidia mzunguko mkubwa wa damu kwa maana hiyo kufanya kuwa na hisia kali za mapenzi kwa hiyo pili pili ni chachu ya kuuamsha hisia 8. Pweza na chaza Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa. Wataalam na wanasayanzi wa ndani kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na wa Kimataifa wamethibitisha kuwa supu ya pweza ina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume. Wataalam hao wanadai kuwa supu hiyo inafanya kazi hiyo kwa asilimia kubwa tofauti na madawa mengine ya kemikali. 9. Chocolate Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid . Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi. 10. Maji ya Kunywa Inapendeza kunywa maji mengi kwa siku na mtu ajitahidi anywe hata zaidi ya lita tanao kama walivyoshauri wataalam wa mambo hayo. Maji pia usaidia kuondoa ugonjwa mwilini na homa za mara kwa mara.tikiti majihusaidia kuamasha hamasa mwili. Kitu gani husababisha uume usimame? Unaweza kujibu ni msisimko. Ni kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi. Hata hivyo msisimko ni matokeo . Kipo kinachosababisha kutokea huo msisimko. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea. Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu sahihi la swali hili ili atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa kuishia. Siyo lazima uwe daktari, Elimu ya kutambua mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama watu wengi mnavyodhani. Kutokusoma soma lolote kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela na hivyo kujikuta tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu. Mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume USIMAME. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU. Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.

Comments

Popular posts from this blog

And this is a true story of the life of Dornald Trump from Hotel developer to president

Do you know 25 amaizing facts about mobile phones